Miaka nenda miaka rudi

Ulinitumia

Halafu ukatimua

Kaniacha mahututi

Sasa unataka rudi

Tuwe marafiki

Wasema nitabarikiwa

Kwani wewe mtumwa?

Mimi hayo mambo siyataki

Achana na michezo

Nenda zako, nenda zako

Nyumba ishafungika

Nilimtupa mwanasesere

Kafungia ushanga

Ndoto za kurudiana

Hatuwezi patana

Kwaheri

Poteza njia

Sahau uhai wangu

Kajifanye msafiri

Kwenye safari sambamba na yangu

Mimi sasa ni buheri wa maendeleo.

Advertisements